PANDA inaweza kusaidia. Piga simu kuhusu wewe mwenyewe au mtu unayemjua.
Mzazi mpya au unatarajia mtoto? Una wasiwasi juu ya unavyohisi?

Orodha ya uchunguzi wa Afya ya Akili
Orodha ya uchunguzi wa Afya ya Akili
Orodha hii inauliza maswali ambayo yanaweza kukusaidia kuelewa vizuri zaidi jinsi unavyohisi, na kama unaweza kufaidika kutokana na usaidizi wa ziada katika ustawi wako ya akili.
Kuhusu PANDA
PANDA inaendesha Simu ya Msaada wa Kitaifa wa Australia ya utaalamu pekee kwa watu walioathirika na wasiwasi na unyogovu wakati wa kuzaa na wendawazimu baada ya kuzaa na kwa wale wanaopata changamoto katika kuwa mzazi.
Pia tunaongeza ufahamu juu ya ugonjwa huu mbaya na wa kawaida ili wale walioathirika waweze kuelewa kinachowatokea na wanaweza kutafuta msaada.
“Nilipokuwa katikati yake nilihisi kama sitapata nafuu tena. Lakini nilipata.”
WAKALIMANI WANAPATIKANA
PANDA ina upatikanaji wa wakalimani kuwasaidia wale ambao hawasemi Kiingereza au wana udhuru wa kusikia au kunena.
“Hakuna mtu aliyeniambia inaweza kutokea hata kabla ya kupata mtoto!”
Wakati wa kupata msaada
Kuwa mjamzito au kuwa mzazi mpya kunaweza kuwa ya kusisimua na changamoto. Kuwa na shida kiasi cha kuzoea mabadiliko ni ya kawaida. Hata hivyo ambapo wakati wa furaha na wa huzuni ya ujumla unakuwa kitu cha hatari zaidi, na kudumu kwa wiki mbili au zaidi, ni wakati wa kupata msaada.
Wasiwasi na unyogovu wa wakati wa kuzaa ni kawaida
Kuna mmoja kati ya mama watano wakitarajia au mama wapya na mmoja katika baba kumi kutarajia au baba wapya watapata wasiwasi au unyogovu wakati wa kuzaa. Inaweza kutokea wakati wa ujauzito (antenatal) au katika mwaka wa kwanza baada ya kuzaa (postnatal). Neno 'perinatal' linahusu zote mbili za ujauzito na mwaka wa kwanza baada ya kuzaa.
“Nina wasiwasi juu ya mpenzi wangu lakini anakataa kuongea nami.”
Wendawazimu baada ya kuzaa
Wendawazimu baada ya kuzaa ni ugonjwa nadra lakini mbaya unaoathiri mmoja hadi mama wawili wapya katika kila mama 1000 na unaweza kumweka mama na mtoto katika hatarini. Karibu daima inahitaji mama kulazwa hospitalini. Dalili mara nyingi hufika ghafla na zinaweza kujumuisha badiliko kali za hisia, mabadiliko makubwa ya tabia na kupoteza mawasiliano na ukweli.
“Mimi ni mama mbaya zaidi duniani.”
Jinsi PANDA inavyoweza kusaidia
Ikiwa wewe ni mzazi anayetarajia au mzazi mpya mwenye wasiwasi juu ya ustawi wako wa kihisia na kiakili - au kuhusu mtu unayemjua - ni muhimu kutafuta msaada. Unapotafuta msaada mapema, unaweza kuanza kujisikia vizuri mapema.
Simu ya Msaada wa Kitaifa wa Afya ya Akili Kabla ya Kuzaa ya PANDA hutoa ushauri wa bure na msaada kwa wazazi wote wapya na wazazi wanaotarajia.
Washauri wetu wenye mafunzo na wanaojali watasikiliza wasiwasi wako na kukusaidia kuchukua hatua za kwanza za kupona.
“Nikimwambia mtu yeyote jinsi ninavyohisi wataona mimi ni mzazi mbaya.”
Ni bora kuzungumza juu ya hiyo
Wasiwasi na unyogovu wakati wa kuzaa ni hali mbaya ya kiafya. Inaweza kuathiri mzazi yeyote mpya au anayetarajia. Si kitu cha kuwa na aibu. Ni vizuri kuzungumza juu yake. Kwa kweli, ni bora uzungumze juu yake!
Kuwaambia wengine kuhusu mapambano yako, au kukubali unahitaji msaada sio ishara ya udhaifu. Inaonyesha kwamba unataka bora kwako mwenyewe na familia yako.
“Nilifikiri ningempenda mtoto wangu papo hapo, lakini siwezi kuvumilia kumtazama.”
Dalili za wasiwasi na unyogovu wakati wa kuzaa
Dalili zinaweza kujumuisha:
- Kuhisi huzuni, chini, au kulia bila sababu dhahiri
- Wasiwasi wa kuendelea wa ujumla, mara nyingi hulenga hofu kwa afya au ustawi wa mtoto wako
- Kuwa na wasiwasi, 'mwenye wahaka', au hofu sana
- Kusumbuliwa kwa urahisi au hasira
- Kujitenga kutoka marafiki na familia
- Matatizo ya kulala, hata wakati mtoto wako anapoalala
- Mabadiliko ya hisia ya ghafla
- Hisia za kuchoka na kukosa nguvu kila wakati
- Dalili za kimwili kama kichefuchefu, kutapika, jasho baridi, ukosefu wa hamu ya kula
- Kuwa na hamu kidogo au hakuna katika mambo ambayo kwa kawaida yanasababisha furaha kwako
- Hofu kuwa peke yako au kuwepo na wengine
- Kupata ugumu wa kulenga, kuzingatia au kukumbuka
- Ongezeko la matumizi ya pombe au madawa ya kulevya
- Mishtuko wa hofu (moyo inapigapiga sana, mipapatiko ya moyo, pungufu wa pumzi, kutetemeka au kuhisi kuwa kando ya kimwili kutoka mazingira yako)
- Kuendeleza tabia za kulazimisha au kutoweza kuacha
- Mawazo ya kifo, kujiua au kumdhuru mtoto wako.
Pia kuna dalili zingine nyingi ambazo hazipo orodha ya hapa. Ikiwa wewe au mtu aliye karibu nawe anapata dalili zozote au hisia ambazo unazo wasiwasi kwa wiki mbili au zaidi, tafadhali tafuta msaada.
“Je, wazazi wote wapya wanahisi mbaya kama hii?”
Piga simu yetu ya bure ya Kitaifa ya
Msaada wa Afya ya Kiakili Wakati wa Kuzaa
Piga simu kwa 1300 726 306
Jumatatu - Ijumaa 9am - 7.30pm AEST / AEDT
Nambari ya Msaada ya Kitaifa ya PANDA inapatikana katika lugha nyingi, pamoja na lugha yako.
Unapopiga simu ya usaidizi ya PANDA, bonyeza chaguo "1" ambalo hutujulisha kuwa unahitaji mkalimani.
Nini kinatokea simu yako inapopokelewa:
Simu yako itajibiwa na mshauri anayezungumza Kiingereza. Tutahitaji kujua lugha unayopendelea - huhitaji kuzungumza Kiingereza isipokuwa kumwambia mshauri lugha unayopendelea.
PANDA itapanga mkalimani na wakati mmoja anapatikana, tutaanza mchakato wa kukusaidia.
Ikiwa mkalimani hayupo, tutakupigia simu.
Kama unahitaji msaada wa haraka piga simu kwa sifuri tatu (000) au idara ya dharura ya hospitali za mitaa.
Ikiwa unahitaji usaidizi nje ya masaa ya kazi ya Simu ya Msaada wa PANDA, piga simu ya Lifeline kwa 13 11 14.
Zoezi la kutuliza
Zoezi hili la kutuliza limeundwa ili kukusaidia kuzingatia kupumua kwako.
PANDA hutoa msaada bure wa ushauri nasaha kwa wazazi watarajiwa na wapya
PANDA hutoa msaada bure wa ushauri nasaha kwa wazazi watarajiwa na wapya.
Ujauzito na kumkaribisha mtoto mpya kunaleta furaha pamoja na changamoto.
Ikiwa unapita wakati mgumu, usiogope kutafuta msaada.
Wewe hauko peke yako; PANDA ipo hapa ili kusaidia ustawi wako wa akili.
Unaweza kupigia simu PANDA kwa 1300 726 306 na mmojawapo wa washauri wetu atakuwapo kukusikiliza. Simu ni bure.
Au unaweza kutembelea kwa www.panda.org.au.
Simu ya Kitaifa ya PANDA (Jumatatu hadi Ijumaa, saa 3 asubuhi hadi saa 1:30 jioni [9am - 7.30pm AEST/AEDT])